Lugha: Kiswahili

Je unaweza kupata mimba kwa kubusiana?

chagua jibu lako [Wakati mwingine] au [Hapana]

Jibu: HAPANA, hauwezi kupata mimba kwa kubusiana. Mimba inaweza kutokea iwapo tu mbegu za kiume zitaingia katika au kumwagikia karibu na uke.

Je mimba inatokeaje/inatungwaje?

  1. Yai (kiini ngono cha kike) lazima litolewe wakati wa upevushwaji wa yai, and
  2. ni lazima kirutubishwe na mbegu ya kiume (kiini ngono cha kiume).

Wakati mvulana na msichana wakifanya ngono bila kutumia kinga, shahawa hutolewa kwenda kwenye uke. Shahawa ni, majimaji mnato meupe ambayo yana mamilioni ya mbegu za kiume ambazo hutoka nje wakati mvulana anatoa shahawa. Hapo ndipo mbegu huogelea katika mirija ya uzazi. Kama msichana akiwa amepevusha yai karibuni (kutolewa kwa yai kutoka katika moja ya ovari zake mbili), kisha mbegu za kiume inaweza kuungana na yai, na hii huleta kitu kinaiitwacho utungisho ambayo huleta mimba.

Kama unataka kujua zaidi kuhusu mimba, wasiliana na [FEMINA HIP (call: +255 222700743, +255 222700742, or send a text to +255 753003001).

Swali linalofuata:

The Internet of Good Things