Lugha: Kiswahili

Je virusi vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI ni kitu kimoja?

Chagua jibu: [NDIO] au [HAPANA]

Jibu: HAPANA. sio kitu kimoja na UKIMWI. VVU ni kifupisho cha maneno: Virusi vya UKIMWI. VVU hushambulia mfumo wa kinga ya mwiliambao hupambana na magonjwa . Bila matibabu, VVU vinaweza kusababisha UKIMWI, ambao ni vifupisho vya maneno Ukosefu wa Kinga Mwilini. VVU huambikizwa kwa njia kuu tano kupitia majimaji ya mwili:

  1. Damu
  2. shahawa,
  3. majimaji ya ukeni,
  4. majimaji kutoka kwenye njia ya haja kubwa na
  5. maziwa ya mama.

Mara mtu anapofikia kuwa na UKIMWI, miili yao inakuwa na wakati mgumu sana wa kupambana na magonjwa mengine. Hii ndio sababu watu wanakufa kutokana na magonjwa yanayohusiana na UKIMWI, lakini si UKIMWI wenyewe.

Chukua hatua:

The Internet of Good Things