Case-Study on Resilience
HADITHI YA UPENDO
Upendo anatoka katika familia ya watoto wane, watatu wakiwa wasichana namvulana ni mmoja. Wazazi wake, Bwana na Bibi Masanja walifariki dunia Upendo alipokuwa na umri wa miaka kumi na mitatu. Kwa vile alikuwa mtoto wa mwisho na mdogo kuliko wote, Upendo alitumia muda mwingi na mama yake ambaye alimfundisha mambo mengi kuhusu maisha. Mara kwa mara mama yake Upendo alimweleza jinsi anavyo amini moyoni mwake kuwa Upendo atakuwa na mafanikio na mara zote alimtia moyo kuwa na uhusiano mzuri na Mungu ambaye atamwongoza. Upendo alithamini sana mapenzi na uhusiano wake na mama yake na alijiaminisha kuwa atakuwa na mafanikio ambayo mama yake anamtakia.

Wakati Bwana na Bibi Masanja walipofariki dunia, waliwaachia watoto nyumba tatu, mbili kati ya hizo zilikuwa zinapangishwa. Hata hivyo, mara tu baada ya wazazi wao kufariki dunia, ndugu waliwanyang’anya hawa watoto nyumba mbili. Upendo na ndugu zake waliachiwa nyumba ndogo sana ya kuishi na hawakupata tena fedha za chakula na za mahitaji mengine ya msingi. Maisha ya Upendo ambaye alikuwa mtoto mdogo kuliko wote, alikuwa na maisha magumu sana. Dada mkubwa wa Upendo aliolewa na hivyo kuondoka nyumbani; dada yake mwingine alipata mpenzi mvulana na muda si muda akapata mtoto wake . Iliamuliwa kuwa Upendo na kaka yake waende kuishi na baba yao mdogo anayeishi katika mji mdogo mwingine. Baba yao mdogo aliwatesa sana na kaka yake akaondoka na kwenda kuishi mitaani.

Upendo alimweleza kiongozi mmoja wa kanisa kuhusu hali hii ambaye alimshawishi kujiunga na klabu ya vijana wa kanisa. Hii ilimpatia fursa ya kuwaeleza watoto wengine matatizo yake- ambao waliokuwa wanaishi katika mazingira magumu.
Katika klabu ya vijana wa kanisa alifanya urafiki na msichana, anayeitwa Furaha, ambaye aliwaeleza wazazi wake hadithi ya Upendo. Wazazi wake Furaha waliguswa na kusumbuliwa na hali ya Upendo na wakaamua kumchukua Upendo ili waishi pamoja nyumbani kwao. Fursa hii ya kupatiwa makazi ilikuja wakati mwafaka kwa kuwa baba mdogo wa Upendo alikuwa ameshamfukuza Upendo kutoka ile nyumba ndogo. Wazazi wa Furaha walimpatia Upendo makazi na malezi na misaada mbalimbali, pia Upendo alipatiwa fursa ya kuhudhuria shule. Upendo anashiriki katika nyanja zote za maisha ya kifamilia na anasaidia katika kazi mbalimbali za nyumbani. Ni hodari wa kujifunza shuleni na ana lengo la kujifunza Sayansi ya Jamii katika Chuo Kikuu ili awe mfanyakazi wa Ustawi wa Jamii na kuwafikia watoto na familia zinazokabiliwa na matatizo katika maisha.

Go back to the training module by clicking on the link below:
Average Rating: ☆ ☆ ☆ ☆ ☆ (0 reviews)
Maoni 6
Tafadhali ingia au fungua akaunti yako
C
CKayumbo
miaka 5 ago
Z
Zabibu
miaka 5 ago
J
janeth
miaka 5 ago
K
Kifovya
miaka 5 ago
A
Alphonce Nicco kwihela
miaka 5 ago