Nalindaje Familia yangu na Uviko 19?
Zifuatazo ni baadhi ya tahadhari wewe na familia yako mnaeza chukua kujisaidia kuepusha maambukizi:
- Osha mikono yako mara kwa mara kutumia sabuni na maji ama sanitaiza iliyo na msingi wa pombe
 - Funika mdomo na pua kwa kiwiko kilicho kunjwa ama karatasi ya shashi unapokohoa ama kupiga chafya. Tupa karatasi ya shashi iliyotumika mara moja.
 - Weka angalau umbali wa mita 1 kati yako mwenyewe na wengine.
 - Mara mingi osha na safisha sehemu zinazoguzwa mara kwa mara kama vile simu, komeo la mlango,swichi za mwangaza na sehemu za juu za kaunta.
 - Tafuta matibabu mapema kama wewe ama mtoto wako mna joto jingi, kukohoa, ugumu wa kupumua ama dalili zingine za COVID-19
 - Epuka maeneo yaliyojaa watu, nafasi zilizofungwa na zilizo na uingizaji duni wa hewa na pia jaribu kujizoesha kukaa kwa umbali unaofaa na watu hadharani.
 - Vaa barakoa za kitambaa ukiwa katika maeneo ya umma ambapo kuna maambukizi ya jamii na umbali wa mwili hauwezekani.
 - Weka nafasi zote za ndani zikiwa na hewa nzuri
 
Average Rating: ☆ ☆ ☆ ☆ ☆ (0 reviews)