Jinsi ya Kuunda Bajeti ya Familia
Bajeti ni nini?
Bajeti ni jinsi tunavyoamua tutakavyotumia pesa, ikiwemo nyakati za matatizo.
Unawezaje kuunda bajeti ya familia?
1. Tafuta jamii yako ikiwa jamii yako inatoa usaidizi.
- Huenda serikali inazipa familia pesa, au vifurushi vya chakula wakati wa janga la COVID-19
- Uliza ikiwa maeneo katika jamii yako yanatoa msaada
2. Unda orodha ya kiasi unachotumia sasa.
- Chukua karatasi na kalamu
- Kiasi cha pesa ambacho familia yako inaweza kutumia kununua chakula na bidhaa nyingine kinaweza kubadilika kila mwezi. Andika kiasi cha pesa ambacho familia yako inaweza kutumia katika mwezi huu!
- Chora picha za bidhaa zote ambazo familia yako hutumia kila mwezi
- Karibu na kila picha andika kiasi cha pesa ya kila bidhaa, na idadi unayohitaji katika mwezi mmoja
3. Zungumzia mahitaji na matakwa.
- Mahitaji: ni bidhaa zipi muhimu au zinazohitajika kwa ustawi wa familia yako? (Mifano: chakula, sabuni ya kunawa mikono, dawa kwa wanafamilia)
4. Unda bajeti yako.
- Tafuta mfuko ulio na mawe au kifaa chochote kilicho na vitonge. Hii ndiyo pesa yako katika mwezi.
- Kwa pamoja, amueni picha zinazoashiria bidhaa mtakazonunua, na muweke mawe kwenye picha
- Ikiwa mnaweza kuhifadhi kiasi cha pesa kwa matumizi za baadaye au dharura—ni bora zaidi!
Asante kwa kusoma! Bonyeza kiungo kilicho hapa chini ili ushiriki maoni yako kuhusu vidokezo hivi vya malezi.