Mabadiliko ya tabianchi husababisha kuenea kwa magonjwa
Watoto hupatwa na magonjwa zaidi yanayotishia maisha yao
Magonjwa yanayoua watoto kwa wingi ulimwenguni (yakiwemo malaria, kuhara na utapiamlo) yanaamshwa kwa urahisi zaidi na hali ya tabia ya nchi, kama vile mafuriko na mabadiliko ya joto.
Kwa hakika, vijidudu vinavyoeneza magonjwa kama vile malaria, homa ya denge na homa yabisi vinaweza kuzaliana zaidi katika maeneo ambako hapo kabla havikuweza kufanya hivyo.
Madimbwi ya maji baada ya mafuriko au kimbunga yanakuwa maeneo ya kuzaliana kwa mbu na kupe, wadudu hawa hivi sasa wanapatikana hata katika nchi za kaskazini ambako hali ya ubaridi haikuwaruhusu hapo kabla kuzaliana.
Zaidi ya hayo, masuala mengine yanayochangia katika mabadiliko ya tabia ya nchi (kama vile utoaji hewa ya ukaa kutokana na magari na viwanda) yanaweza kabisa kudhuru afya ya watoto. Kwa mfano, vifo kutokana na pumu, ambao ndio ugonjwa ulioenea sana miongoni mwa watoto, vinatarajiwa kuongezeka sana labda hatua madhubuti za haraka zichukuliwe hivi sasa.