Miti inasaidia kukabili mabadiliko ya tabianchi
Ufyekaji misitu huathiri watoto, hasa wasichana
Miti hutukinga dhidi ya joto la mchana, huzaa matunda tunayokula na kuongeza uzuri wa mandhari. Kukata miti kwa ajili ya kuni kunasababisha upotevu wa misitu na jangwa na kunahusishwa na utoaji hewa ya ukaa na kusababisha mabadiliko ya tabia ya nchi.
Kwa mtazamo wa kimazingira, miti ni muhimu: oksijeni ambayo ni muhimu kwa uhai inazalishwa na miti na huondoa uchafuzi wa hewa, inapunguza ukali wa joto na kuongeza unyevunyevu katika hewa. Miti huzuia udongo usipukutike na kupunguza mtiririko wa maji ardhini, miti huzuia mmomonyoko wa udongo, hudhibiti maporomoko ya barafu, huzuia kuenea kwa jangwa, hulinda fukwe na kupunguza uhamaji wa milima ya mchanga. Ndege na viumbe hai vingine vinahitaji miti kwa ajili ya makazi na chakula—na hata watoto pia.
Zaidi ya hayo, uharibifu wa miti ni pia suala la jinsia na afya. Wanawake na wasichana wanatumia muda mwingi zaidi kutafuta kuni, na pia hujiweka katika hatari kubwa sana kwa sababu ya moshi wanapokuwa jikoni wakipikia kuni.
Utunzaji mazingira kwa kupanda miti ni moja ya misingi ya maendeleo. Kwa mfano, Serikali ya Ethiopia iliweka lengo la kupanda miti milioni 20. Mashirika ya Umoja wa Mataifa yalishirikiana kwa karibu na serikali ili kuhimiza umma, hasa watoto na vijana, kushiriki katika changamoto hii.