talking to children about covid.png

Kuzungumza na watoto kuhusu Uviko-19

Kuwa tayari kuzungumza. Tayari watakuwa wamesikia kitu. Ukimya na siri hazilindi watoto wetu. Bali uaminifu na uwazi. Fikiria kuhusu ni kiasi gani wataelewa. Unawajua zaidi.

Kuwa wazi na usikilize Ruhusu mtoto wako azungumze kwa uhuru. Waulize maswali ya wazi na ujue ni kiasi gani tayari wanajua.

Kuwa mwaminifu Daima jibu maswali yao kwa ukweli. Fikiria kuhusu umri wa mtoto wako na ni kiasi gani anaweza kuelewa.

Kuwa msaada Mtoto wako anaweza kuogopa au kuchanganyikiwa. Wape nafasi ya kushiriki jinsi wanavyojisikia na wajulishe uko kwa ajili yao.

Ni sawa kutokujua majibu Ni vizuri kusema ""Hatujui, lakini tunashughulikia; au hatujui, ‘lakini tunafikiria’. ” Tumia hii kama fursa ya kujifunza kitu kipya na mtoto wako!

Mashujaa sio waonevu Eleza kuwa COVID-19 haihusiani na jinsi mtu anavyoonekana, ametoka wapi, au ni lugha gani anazungumza. Mwambie mtoto wako kwamba tunaweza kuwa na huruma kwa watu ambao ni wagonjwa na wale wanaowahudumia.

Tafuta hadithi za watu ambao wanafanya kazi ili kuzuia kuzuka na wanawajali wagonjwa.

Mwisho kwa Ujumbe Mzuri Chunguza kuona ikiwa mtoto wako yuko sawa. Wakumbushe kwamba unajali na kwamba wanaweza kuzungumza nawe wakati wowote. Kisha fanya kitu cha kufurahisha pamoja!

Msomee Mtoto wako Msomee mtoto wako hadithi kuhusu watoto wanaokabiliwa na COVID-19 duniani kote hapa:

Ifuatayo