student tool kit_having fun at home.png

Kuwa na Furaha Nyumbani

Hapa kuna maoni ya vitu unavoweza fanya nyumbani ambazo zinahitaji vifaa vichache sana na ambazo zitafanya wakati wa nyumbani kuwa wa kufurahisha zaidi!

Having Fun at Home 2

Hadithi katika Picha

  • Fikiria hadithi unayofurahi kusikia au kuhadithia. Inaweza kuwa hadithi ya kweli, hadithi ya jadi, au hadithi unayotengeneza.
  • Fikiria mandhari sita muhimu katika hadithi, pamoja na mwanzo na mwisho.
  • Kunja karatasi katika mraba sita. Chora mandhari hizo sita muhimu kwenye masanduku.
Having Fun at Home 3

Tafuta Ushairi

  • Tumia siku kusikiliza vitu watu walio karibu na wewe wanasema. Andika maneno, misemo au sentensi unazosikia.
  • Unda shairi kwa kuweka maneno, misemo au sentensi pamoja kwa mpangilio wowote unaopenda.
Having Fun at Home 4

Kopo la Furaha

  • Pata ujumbe chanya juu wa maisha na furaha kutoka kwa vitabu ambavyo umevisoma, vijana au watu wazima katika jamii. Ongeza maoni yako mwenyewe ya ubunifu kwa ujumbe chanya.
  • Andika kila ujumbe kwenye karatasi ndogo na uweke kwenye kopo.
  • Kila asubuhi vuta nukuu moja kutoka kwenye kopo na ujisomee mwenyewe au wengine
Having Fun at Home 5

Kusanya tena Mosaiki

  • Tafuta majarida na magazeti ya zamani, mifuko ya plastiki ya rangi tofauti, au chakavu cha kitambaa.
  • Kata katika miraba midogo, angalau 1cm/1cm.
  • Tengeneza picha kwa kugundisha miraba kwenye kipande cha karatasi
Having Fun at Home 6

Fikiria Mahali Bora

  • Chagua mahali katika jamii yako.
  • Fikiria nini kingepafanya pawe mahali bora kwa vijana.
  • Chora picha kuonyesha maono yako.
Having Fun at Home 7

Fikiria Uvumbuzi

  • Fikiria juu ya shida unayokumbana nayo kila siku. Inaweza kuwa shida kubwa au shida ndogo.
  • Fikiria uvumbuzi ambao ungefanya shida kuwa bora au kuisuluhisha.
  • Chora mchoro wa uvumbuzi uliyowaza. Andika maelezo ili watu wengine waweze kuelewa jinsi ingefanya kazi.
Having Fun at Home 8

Jicho la Ndege na Jicho la Mdudu

  • Fikiria mahali katika jamii yako panavyoonekana kupitia macho ya ndege anayeruka juu au ameketi juu ya mti. Chora picha ya kile angekiona.
  • Fikiria mahali sawa kutoka kwa mtazamo wa mchwa au mbawakawa amesimama ardhini. Chora picha ya kile angeona.
Having Fun at Home 9

Picha ya Fremu

  • Tafuta vijiwe, chakavu ya karatasi au plastiki, gundi, na vipande vikubwa vya mstatili vya karatasi au gazeti.
  • Gundisha vijiwe, chakavu au karatasi au plastiki karibu na mpaka wa vipande vikubwa vya mstatili wa karatasi. Wacha ikauke.
  • Kata katikati ya karatasi na itumie kama muafaka wa picha
Iliyotangulia Ifuatayo