Kucheza na kuwasiliana na watoto wa mwaka mmoja hadi miaka miwili!
Watoto wachanga hutembea sana!
JE WAJUA?
-
Endapo watoto wachanga wakiwa na afya nzuri na wakilishwa vizuri, wanakuwa wachangamfu zaidi.
-
Watoto wachanga hujifunza kwa kuanza kuyaelewa maneno na ndipo huanza kuyazungumza.
-
Watoto wachanga hufurahia kucheza na vitu rahisi kutoka majumbani au vitu vinavyotokana na asili, na hawana haja na midoli ya kununua madukani.
-
Watoto hupendelea kufungua kurasa wakiwa wanaangalia vitabu. Pia wanao uwezo wa kukumbuka vitu kama ukitaja majina ya vitu wanavyovikumbuka.
-
Watoto wachanga wanahitaji hamasa kama wakianza kujaribu kutembea, kucheza michezo mpya, na kujifunza ujuzi mpya.
-
Wakati wachanga wanapoanza kujifunza mchezo mpya au ujuzi mpya, huwa wanarudia tena na tena.
-
Watoto wachanga huwa wanapenda kuweka vitu katika makopo na masanduku, na kisha kukitoa nje.
-
Watoto wachanga hufurahia hasa wanapoona kwamba wanawafanya watu wazima waliowazunguka kuwa na furaha pia.
Makala inayofuata: