iogt vectors 3_play and comms with toddlers.png

Kucheza na kuwasiliana na watoto wa mwaka mmoja hadi miaka miwili!

Watoto wachanga hutembea sana!

JE WAJUA?

  • Endapo watoto wachanga wakiwa na afya nzuri na wakilishwa vizuri, wanakuwa wachangamfu zaidi.

  • Watoto wachanga hujifunza kwa kuanza kuyaelewa maneno na ndipo huanza kuyazungumza.

  • Watoto wachanga hufurahia kucheza na vitu rahisi kutoka majumbani au vitu vinavyotokana na asili, na hawana haja na midoli ya kununua madukani.

  • Watoto hupendelea kufungua kurasa wakiwa wanaangalia vitabu. Pia wanao uwezo wa kukumbuka vitu kama ukitaja majina ya vitu wanavyovikumbuka.

  • Watoto wachanga wanahitaji hamasa kama wakianza kujaribu kutembea, kucheza michezo mpya, na kujifunza ujuzi mpya.

  • Wakati wachanga wanapoanza kujifunza mchezo mpya au ujuzi mpya, huwa wanarudia tena na tena.

  • Watoto wachanga huwa wanapenda kuweka vitu katika makopo na masanduku, na kisha kukitoa nje.

  • Watoto wachanga hufurahia hasa wanapoona kwamba wanawafanya watu wazima waliowazunguka kuwa na furaha pia.

Makala inayofuata:

Iliyotangulia Ifuatayo