Kucheza na watoto wa mwaka mmoja hadi miaka miwili!
Watoto wanakuwa na kujifunza haraka sana
UNACHOWEZA KUFANYA NA KUCHUNGUZA
- Mpe mtoto wako vitu aviweke katika makopo au masanduku, na kisha akitoe nje.
Yeye atajaribu kuvitoa vitu na kuvirudisha mwenyewe ndani ya sanduku, hili ni jambo jema kwa ajili ya kukuza namna macho yake inahusiana na mikono yake.
- Mpatie mtoto wako vitu vya kukusanya kimoja juu ya kingine.
Yeye atajaribu kukusanya vitu vingi zaidi mwenyewe na kuviangusha au atavikusanya vitu kimoja juu ya kingine mpaka vitakapoanguka.
- Muulize mtoto wako maswali marahisi na umjibu pale mtoto anapojitahidi kuongea.
Yeye atakuwa na nia kushirikiana kwa kukujibu na/au kukuuliza maswali zaidi.
- Jaribu kuongelea uhalisia wa aina mbali mbali na mtoto wako, kama vile asili, picha na vitu vilivyo kwenye mazingira yaliyowazunguka.
Unapaswa kuona mtoto wako akizunguka na kuonesha nia ya kuchunguza mazingira.
- Muhamasishe mtoto wako ajifunze kwa kuangalia anachokifanya na kukitaja: “Unajaza masanduku.”
Yeye atafurahia kukuonyesha alichojifunza na atazidi kujithamini.
- Cheza na mtoto wako na umpatie msaada: “Tufanye pamoja. Haya hapa ni mawe ya kuweka kwenye sanduku lako”.
Kuvumbua vitu hivi kutamfanya afurahi na kutamuongezea hali ya kujiamini.
- Tumia kila nafasi unayopata ya kushiriki katika mazungumzo na mtoto wako, hii ni pamoja na wakati kumlisha au kumwogesha, au wakati wa kufanya kazi ukiwa karibu na yeye.
Yeye karibuni ataanza kuelewa unachokisema na ataweza kufuata maelekezo rahisi.
- Unaweza kucheza michezo rahisi ya maneno, na kumuuliza maswali marahisi: "Kidole chako cha mguuni kipo wapi?" au “Ndege yuko wapi?”. Mnaweza kuangalia picha na mkajadiliana kuhusu mnachokiona.
Yeye atazidi kuonyesha udadisi zaidi na zaidi na nia ya kuwasiliana juu ya nini ambacho yeye anakiona na kukisikia.
-