Kucheza na kuwasiliana na watoto wa miaka miwili + watoto wadogo
Kuainisha, kuhesabu na kuongea!
-
Watoto wanajifunza kuvipa vitu majina, kuainisha na kuhesabu.
-
Watoto wanaojifunza kuongea hufanya makosa mengi. Hata hivyo kuwarekebisha, kutawakatisha tamaa ya kuongea.
-
Hadithi, nyimbo, na michezo huwandaa watoto kusoma na kuwasaidia kuboresha jinsi wanavyoongea.
-
Hadithi za jadi, nyimbo, na michezo inasaidia kuwafunza watoto namna ya kuishi.
-
Watoto wanaweza kujifunza kuongea kwa usahihi - kwa kusikiliza watu wengine wanaoongea kwa usahihi.
-
Watoto wanaweza kujifunza na kuelewa kipi ni kizuri na kipi ni kibaya.
-
Pia watoto huwa wanaiga yanayofanywa na kaka, dada na ndugu wengine kwa sababu wangependa kujua ni kipi kizuri na ni kipi kibaya.
-
Watoto hujifunza vyema kama wakifundishwa namna ya kuishi vyema badala ya kukaripiwa wanapofanya kufanya vibaya.
Makala inayofuata: