iogt vectors 3_playing with child.png

Kucheza na watoto wenye zaidi ya miaka miwili.

Watoto wachanga wanaweza kushughulikia mambo magumu zaidi.

UNACHOWEZA KUFANYA NA KUCHUNGUZA

  • Uliza maswali rahisi na kusikiliza majibu. Muhamasishe mtoto wako kuzungumza: "Je, hichi ni nini?" "Dirisha lipo wapi?" "Mpira upi ni kubwa?" “Je, ungependa kikombe chekundu?”

Unapaswa kuona hamasa ya mtoto wako ikikuwa katika mazungumzo na wewe huku akijaribu kujibu maswali yako.

  • Soma hadithi kwa mtoto wako na umuulize maswali juu ya nini vitu vinavyoonekana kwenye kitabu.

Utagundua Kwamba mtoto wako anakariri na kujaribu kurudia ulichokisoma.

  • Tengeneza midoli rahisi kama vile vitu vya rangi tofauti na maumbo ya kuainisha, fimbo au ubao wa chaki, fumbo.

Mtoto wako atakuwa anajifunza kutokana na ulichokitengeneza na ataifurahia zaidi midoli unayoitengeneza.

  • Msaidie mtoto wako kujifunza kuhasebu kwa kumuuliza “ziko ngapi” na kuhesabu pamoja nae.

Mtoto wako atafanya makosa mwanzoni, lakini atajifunza kwa kurudia vitu mara kwa mara.

  • Mpatie mtoto wako maduara na maumbo mengine yaliyokatwa kwenye karatasi zilizopakwa rangi ayatofautishe na kuyaainisha.

Atafurahia kuweza kuainisha vitu na atajifunza jinsi ya kulinganisha na kujenga mahusiano baina ya vifaa, rangi na maumbo.

  • Muhamasishe mtoto wako kuongea na ujibu maswali ya mtoto.

Unatakiwa uchunguze kuwa mtoto wako anaweza kuelewa na kushughulikia mambo zaidi na zaidi yaliyo magumu.

Makala inayofuata:

Iliyotangulia Ifuatayo