iogt vectors 3_useful tips for 1-2 years copy 2.png

Dondoo muhimu kwa ajili ya watoto wa miaka miwili + watoto wadogo

Kucheza pamoja.

DONDOO NA MIDOLI AMBAYO UNAWEZA KUTUMIA KWA AJILI YA WATOTO WA MIAKA MIWILI + WATOTO WACHANGA

  • Fanya hesabu yoyote unayofanya na mtoto kwa furaha. Ziimbe namba. Wasaidie kugusa au kushika vitu pindi mnapovihesabu.

  • Jaribu - kwa subira - kujibu maswali ya mtoto kadri uwezavyo.

  • Jitahidi usiongee maongezi yanayopingana na mtoto wako. Maada inapokuwa ipo sahihi unapofanya maongezi na mtoto inasaidia kuendeleza fikra za mtoto kwa urahisi.

  • Kumbuka watoto huweka taarifa ya kila unachosema. Unavozidisha kukisema kitu, ndivo watavokikumbuka kwa uharaka kinamaanisha nini.

  • Kwa nyakati zote ni bora kumrekebisha mtoto wako kwa njia ambayo haitamfanya aone haya. Watoto bado wanafurahia kucheza na midoli ya kawaida iliyotengenezwa nyumbani. Hawahitaji midoli ya kununuliwa madukani.

  • Watoto wanaweza kujifunza kuchora kwa chaki kwenye jiwe au kwa kijiti kwenye mchanga.

  • Unaweza kutengeneza mafumbo kwa kukata magazeti au picha rahisi kuwa vipande vikubwa.

  • Watoto wanajifunza kulinganisha rangi, maumbo na ukubwa kwa vifaa rahisi, kama vile vizibo vya chupa.

  • Kukusanya mbegu: Chukua pande la mbao na fimbo (fimbo isiwe na ncha sana au nyembamba sana). Gundisha fimbo kwenya mbao. Kusanya mbegu kuanzia tano mpaka kumi za urefu tofauti na ukubwa tofauti. Toboa tundu katika kila mbegu, na uipake kila mbegu rangi tofauti.

Makala inayofuata:

Ifuatayo